KESI ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, inatarajiwa kuendelea leo Jumatatu,tarehe 8 Septemba 2025, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, isikilizaji huo utakuwa wa awali (Preliminary hearing)chini ya uongozi wa Jaji Dunstan Nduguru. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Awali shauri hilo liliwasilishwa katika Mahkama ya Hakimu Mkazi Kisutu kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa hatua zaidi za kisheria. Kesi imeahirishwa mara kadhaa kutokana na sababu mbalimbali za kitaratibu na maandalizi ya pande husika.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa usikilizaji wa awali kufanyika katika ngazi ya Mahakama Kuu tangu shauri hilo kupelekwa huko,ambapo pande zote zinatarajiwa kuwasilisha hoja zao za awali kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
ZINAZOFANANA
Machafuko ya 29 Oktoba: Maaskofu Katoliki wataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wawajibike
Shinikizo la kufanyika uchunguzi wa mauaji ya 29 Oktoba lashika kasi
Meridianbet yaendelea kuwekeza kwa jamii kupitia MRC Rehabilitation Centre