
Rais Samia Suluhu Hassan
MGOMBEA wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan, amesema ni dhamira yake kuwa kabla hajaondoka madarakani awe amefanikisha upatikanaji wa Jengo la Machinga (Machinga Complex) Iringa Mjini kama sehemu ya kutekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).
Samia ameyasema hayo hii leo Jumapili tarehe 7 Septemba 2025, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Samora Iringa mjini.
Mgombea huyo amesema kuwa tayari serikali kupitia Wizara ya TAMISEMI imejenga Jengo la Ofisi za Machinga Mkoani humo kama sehemu ya kurahisisha uratibu na ufanyaji kazi wa kundi hilo la wafanyabiashara wadogo kwenye Mkoa huo wa kusini Magharibi mwa Tanzania.
“Hatujawasahau wafanyabiashara wadogo, ambapo wakati ule niliahidi kujenga soko la Machinga. Niwaambie Kwamba eneo limeshatengwa ambalo lilikuwa stendi ya mabasi, na sasa tumeanza utaratibu wa kukusanya fedha za kujenga Machinga Complex ndani ya Mji wa Iringa.
Ni hamu yangu nimalize kabla kumalizia muda wangu wa kazi, nataka nimalize Machinga Complex ndani ya Iringa na wanangu wale wamachinga wamamalishe na wengine wote waweze kufanya biashara zao,” amesema Samia
Katika hatua nyingine Samia ameeleza mafanikio yaliyopatikana kwenye awamu yake ya kwanza kama Rais wa Tanzanka ikiwa ni pamoja na maboresho ya uwanja wa ndege Iringa, Ujenzi wa barabara ta Mchepuko (Iringa bypass) ambayo ujenzi wake umefikia asilimia tano, akiahidi pia kuendelea kujenga miundombinu ya barabara za kiwango cha lami katika Mji wa Iringa ikiwa wananchi watampa ridhaa ya kuongoza tena kwa kipindi cha pili.
ZINAZOFANANA
Mkituchagua tena tutaendelea kutoa ruzuku ya mbolea
Samia ajivunia ahadi zake za nyuma
Rais Mwinyi akemea kauli za uchochezi