September 6, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Bosi wa JamiiForum ajiuzulu ujumbe wa Tume ya Ulinzi ya Taarifa Binafsi

Maxence Melo

 

MKURUGENZI wa Jamii Forums, Maxence Melo amejiuzulu nafasi yake ya Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,hatua inayokuja ikiwa ni takribani miaka miwili tangu ateuliwe kuchuka nafasi hiyo. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Melo ambaye aliteuliwa kushika nafasi hiyo mnamo tarehe 18 Desemba 2023, ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

“Leo tarehe 6 Septemba 2025, nimemuandikia rasmi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari juu ya uamuzi wangu wa kujiuzulu ujumbe wa Bodi katika Tume ya Ulinzi Taarifa Binafsi”.

“Aidha, naishukuru Taasisi yangu na Bodi ya Wakurugenzi kwa kulipa gharama zote za ushiriki wangu katika vikao vyote na shughuli za Tume kwa takribani miaka miwili,” ameandika Melo.

Hatua ya Maxence kujiuzulu imekuja muda mfupi baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kutangaza kusitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums pamoja na kuzuia upatikanaji wa Jukwaa lake.

About The Author

error: Content is protected !!