
Maxmillian Machumu 'Mwanamapinduzi'
ASKOFU Maxmillian Machumu ‘Mwanamapinduzi’ ameiambia MwanaHALISI kuwa amekimbia nchi kwa kile alichoeleza anasakwa kwa lengo la kuawa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mwanamapinduzi amesema kuwa amejiridhisha kuwa anasakwa kwa lengo la kutekwa kutoka kwenye vyanzo vya uhakika.
“Nimepokea taarifa kutoka kwenye vyanzo vya uhakika kuwa mimi na Askofu Josephat Gwajima tunasakwa kwa ajili ya kutekwa na kuuawa … mara nyingi nimekuwa nikifuatiliwa na kukimbizwa na magari mbalimbali katika mazingira tata” alisema kwenye waraka wake.
Askofu Mwanamapinduzi hajasema yupo nchi gani lakini amesema kuwa hayupo nchini kwa ajili ya kujinusuru.
ZINAZOFANANA
Msaidizi wa Mafwele aanza kutoa ushahidi kesi ya Lissu, kesho zamu yake kumbanwa
Mawakili wa Polepole watoa tamko
Lissu asimamisha mahakama kisa tarehe ya hukumu yake kabla ya kusikilizwa