
MGOMBEA Urais kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali yake itanunua meli kubwa ya uvuvi itakayosaidia shughuli za uvuvi na kuongeza kipato cha wavuvi. Amaripoti Mwandishi Wetu, Pangani, Tanga … (endelea).
Doyo amesema hayo leo, terehe4 Septemba 2025, akiwa katika viwanja vya Stendi ya Pangani, Tanga, akifungua kampeni za chama chake kitaifa na kuwaomba Watanzania kumchagua kuwa Rais.
Katika sera zake, Doyo amesema chama chake kikichukua dola kitahakikisha rasilimali za nchi zinatumika kuboresha maslahi ya Watanzania na kuzisimamia kikamilifu ili kuwa na tija katika uzalishaji wa rasilimali hizo,ikiwa ni pamoja na madini na misitu.
Doyo na timu yake wameanza kampeni hii leo na wanatarajia kuzunguka nchi nzima kuomba ridhaa ya Watanzania kuwachagua kwa kwa kipindi cha miaka mitano ya 2025-2030 kuongoza nchi.
ZINAZOFANANA
Bwege adai kutaka kuhongwa Sh. 100 milioni kuivuruga ACT
Rais Mwinyi azindua kituo cha mabasi na soko la Chuini
Matibabu bure ya Moyo, Figo na Sukari kwa wasiojiweza sio kila mtu – Samia