
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu 10 kwa tuhuma za kukutwa wakitumia namba za SSH 2530 kwenye magari. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni sehemu ya utekelezaji onyo la kutotumia namba hizo baada ya tarehe 1 Septemba 2025.
Awali, Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Msemaji wake David Misime, lilipiga marufuku matumizi ya namba hizo kwenye magari na kutoa hadi tarehe 1 Septemba wahusika wawe wamezitoa.
Alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakibandika namba hizo kwenye magari yao kinyume cha sheria, jambo ambalo lilizua sintofahamu kwa watumiaji wengine.
“Mtu yeyote anayebandika namba hizo baada ya kufuatiliwa kwenye mifumo ya usajili, itahesabika hilo ni kosa la kisheria na atakayematwa atakuwa na kosa la kuendesha chombo cha moto bila usajili wa namba rasmi,” alisema Misime.
Leo tarehe 4 Septemba 2025 Kamanda wa Kanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu 10 huku msako ukiendelea.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 13(!) cha Sheria ya Usalama Barabarani,Sura ya 168 Marejeo ya Mwaka 1973 yaliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023, mtu yeyote anayeendesha chombo cha moto bila kuwa na usajili rasmi na namba halali za usajili anatenda kosa la jinai.
ZINAZOFANANA
Bwege adai kutaka kuhongwa Sh. 100 milioni kuivuruga ACT
Rais Mwinyi azindua kituo cha mabasi na soko la Chuini
Matibabu bure ya Moyo, Figo na Sukari kwa wasiojiweza sio kila mtu – Samia