
Suleman Bungara 'Bwege'
ALIYEKUWA Mbunge wa Kilwa kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Suleman Bungara ‘Bwege’ amesema kuwa kuna baadhi ya wanachama na viongozi wa upinzani wanatumika kuvihujumu vyao ili kunufaisha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Amedai kuwa hata hatua ya Monalisa Ndala kuwasilisha malalamiko kwa msajili wa vyama vya siasa nchini, juu ya kukosewa kwa kanuni za uchaguzi wa Chama cha ACT- Wazalendo kwa kumpitisha Luhaga Mpina kuwa mgombea urais wa chama hicho ni mpango wa kudhoofisha upinzani.
Hata hivyo Monalisa amekana madai ya kutumiwa kuvuruga chama chake bali anafanya hivyo kulinda, kutetea katiba na kanuni za chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, tarehe 4 Septemba 2025, jijini Dar es Salaam, Bwege amesema uamuzi wa msajili wa vyama vya siasa kusema kuwa Mpina sio mgombea halali wa chama hicho na baadaye Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ni uthibitisho wa mbinu za kuua upinzani.
Mwanasiasa huyo amesema kuwa yeye aliyewahi kutafutwa na mtu mmoja (jina tunalihifadhi) alimuahidi fedha ili avuruge uchaguzi wa ACT Wazalendo uliofanyika tarehe 5 Machi, 2024.
Bwege amesema yanayoendelea hivi sasa hayamridhishi kwa kuwa anaona demokrasia inavyobagazwa.
Tarehe 2 Machi 2024 Bwege anasema kuwa akiwa nyumbani kwake Kilwa alipigiwa simu na mtu huyo aliyemuomba afike jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.
“Nikamuuliza nakujaje akaniuliza unayo gari nikamwambia gari ninayo akamwambia basi nitakutmia hela ya mafuta basi muda ule ule akatuma shilingi laki tano na kunitaka siku ile ile nije Dar es Salaam”
Bwege anasema kuwa siku ile ile alilazimika kusafiri na kufika Dar es Salaam sita usiku “nikampigia simu akasisitiza kuwa leo leo nataka tukutane mpaka nikapata wasiwasi labda ni mtego wa watu wasiojulikana ikabidi nimuombe mwanangu ambaye anaishi hapa Dar es Salaam anisindikize basi akuteelekeza mpaka kwake tukafunguliwa mlango na kusema kweli yule mtu ana muonekano wa kisheikh”
Bwege anasema kuwa yule Sheikh akaanza kumwambia aliokusudia “N imesikia kuna uchaguzi ndani ya chama chenu cha ACT-Wazalendo unafanyika tarehe 5 nikamjibu kweli upo akasema kama kuna uchaguzi kwa hali iliyokuwepo kwenye Uchaguzi unaompambanisha Juma Duni na Othman Masoud Othman kwenye nafasi ya uenyekiti sasa Duni atafedheheka hali atashindwa uchaguzi atapata kura kidogo mno nikamwambia mimi najua”
Bwege ameendelea kusema kuwa yule mtu akamwambia dhumuni la yeye kumuita usiku huo wa saa saba ni kutaka kufanya mpango wa kuhakikisha huo uchaguzi haufanyiki.
“Tunataka tumuokoe Babu Duni asifedheheke nikamuuliza tunamuokoaje akasema kuokoa kwake kutatokana na wewe kama utatukubalia akasema sisi tunataka kuuharibu uchaguzi tarehe 5 kusiwepo uchaguzi nikamuuliza tunauharibuje?
“Akajibu kuna watu wanapiga kura huko vijijini kwenye matawi hawakulipa ada na kama hawakulipa ada sio wanachama kwa hiyo sisi tunataka tuipeleke kesi mahakamani kwa sababu uchaguzi mchakato wake haukuwa huru na wa haki kwa hiyo wewe tumekuita kwa kuwa mtu mwenye haki ya kushtaki na kushtakiwa kwenye chama ni bodi ya wadhamini
“Kwa hiyo wewe na mkeo kwa ni mjumbe wa bodi ya wadhamini tunataka aende mahakamani kukishtaki chama cha ACT-Wazalendo kwa kuendesha kikao kinyume na utaratibu nikawaambia ndio mke wangu Mwanawetu Said ambaye nimezaa naye watoto watatu ni mjumbe wa bodi ya wadhamini.
Bwege amesema mazungumzo yao yalihitimishwa na malipo kutokana na kazi hiyo .
“Mkeo akitia sahihi mashtaka yetu tutakupa Sh. 100 milioni na tutakupa kabla hajatia sahihi na akaniambia kabisa kwamba hili jambo limebarikiwa na mtu mzito serikalini wakaniambia watanilinda ”
Bwege anasema kuwa jambo alipolifikisha kwa mkewe aligoma kufanya kazi hiyo na tukamwambia kama kweli ametumwa na mtu mzito basi tumuone huyo mtu mzito.
Amesema mtu huyo alimpigia simu na yeye (Bwege) akamwambia amkutanishe na huyo kigogo lakini hakukubaliana naye hivyo walishindwana.
Bwege anasema kuwa baada ya yeye na mke wake kukubaliana kukutaa kushiriki mchezo huo na kwa kuwa mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo haukuchelewa kufanyika zoezi hilo lilikwama na kukiacha chama salama.
ZINAZOFANANA
Msako wa magari yenye namba za usajili SSH 2030 wasaka 10 Dar
Rais Mwinyi azindua kituo cha mabasi na soko la Chuini
Matibabu bure ya Moyo, Figo na Sukari kwa wasiojiweza sio kila mtu – Samia