
MGOMBEA wa kiti cha Urais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, mzigo wa gharama za matibabu ambao serikali utabeba kwa baadhi ya magonjwa utalenga wananchi wasiojiweza na sio kila mtu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe … (endelea).
Rais Samia ameyasema hayo hii leo tarehe 3 Septemba 2025, katika muendelezo wa kampeni mkoani Songwe kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Mgombea huyo alisema kuwa wakati anazindua kampeni jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, alitoa ahadi ya bima ya Afya kwa wote, sambamba na serikali kubeba mzigo wa matibabu na vipimo kwa baadhi ya magonjwa lakini ni kwa watu wasio jiweza tu.
“Wakati nikizindua kampeni nilitoa ahadi ya bima ya afya kwa wote, lakini nilisema kuna magonjwa serikali itabeba mzigo, hii nilisema kwa wale ambao hawatakuwa na uwezo, sio kila mtu.” Alisema Rais Samia
Aidha alisisitiza kuwa, lengo ni kwa watu wasiokuwa na uwezo na kama mtu akithibitishwa Serikali itababe mzigo huo.
“Lengo ni kwa wasiokuwa na uwezo, tukithibitisha serikali itabeba mzigo wamatibabu,” alisisitiza Rais Samia
Ikumbukwe katika uzinduzi wa kampeni Rais Samia alitoa ahadi ya kuwa ndani ya siku 100 za mwanzo atahakikisha sheria ya bima ya afya inazinduliwa ambapo wataanza na makundi.
“Makundi tutatakayoanza nayo ni wazee, wajawazito, watoto na makundi mbalimbali ambapo gharama zao zitabebwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Gharama za matibabu zitabebwa na mfuko huo
Rais Samia alisema pia Serikali itaanza kugharimia matibabu ya kibingwa kwa watu wasijiweza ambayo yamekuwa yakiwafanya watu wshindwe kumudu gharama zake.
“Tutagharimia magonjwa ya saratani, figo, moyo na mifupa ya yale ya fahamu ambayo wananchi wanashindwa kumudu gharama zao. Pia tutaajiri wahudumu wa sekta ya afya 5000” alisema.
ZINAZOFANANA
Wenje aibuka, aunga mkono kususia uchaguzi
Mbunge aliyekaa siku 8 ACT-Wazalendo arudi CCM
Nchimbi amfungulia Mpina mlango wa kurejea CCM