
HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje, amejitokeza hadharani na kupinga uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Wenje amekuwa kimya tangu aliposhindwa na John Heche kwenye kinyang’anyiro cha kuwania umakamu mwenyekiti wa Chadema katika uchaguzi uliofanyika tarehe 22 Januari 2025, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kuwasikiliza wananchi.
“CCM watalipa gharama, sisi tuendelee kupigania mabadiliko, wafuasi wa Chadema na wananchi tuendeleze mapambano ya kudai mabadiliko ya kisiasa na kikatiba nchini”
Chadema kimekataa kushiriki uchaguzi wa mwaka huu hadi mabadiliko ya sheria na mifumo ya uchaguzi ifanyike.
ZINAZOFANANA
Mbunge aliyekaa siku 8 ACT-Wazalendo arudi CCM
Nchimbi amfungulia Mpina mlango wa kurejea CCM
Wasira: Kazi aliyoifanya Rais Samia anastahili kuchaguliwa tena