BAADA ya siku nane za kukaa ndani ya chama cha ACT-Wazalendo aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini mkoani Manyara,Flatei Gregory Massay, amerejea tena Chama Cha Mapinduzi (CCM. Anaripoti Fedrick Gama, Dar es Salaam … (endelea).
Massay aliyejiunga na ACT-Wazalendo tarehe 25 Agosti 2025 baada ya jina lake kukatwa kwenye mchakato wa uteuzi wa wanaowania ubunge alihamia chama hicho cha upinzani na kuchukua fomu za kutetea kiti chake.
Mwanasiasa huyo atakumbukwa kwa kitendo cha kuruka sarakasi ndani ya ukumbi wa Bunge wakati akichangia hoja kutilia uzito wa kile alichokuwa akikichangia kwenye hoja ya kutaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ijenge barabara iliyoahidi kuijenga katika jimbo lake.
ZINAZOFANANA
AG Zanzibar aweka mapingamizi kesi za Uwakilishi
Butiku aita Wazee kujadili ya 29 Oktoba
Kesi ya uhaini ya Lissu kusikilizwa siku 26 mfululizo