August 19, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kesi ya Lissu yapelekwa Mahakama Kuu.

Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema akiwa mahakamani Kisutu

 

KESI ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu imehamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo imeamishwa kwenye Mahakama hiyo, mara baada ya Lissu kusomewa kusomewa maelezo ya mashahidi (Committal) mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franko Kiswaga.

Hata hivyo, awali majira ya asubuhi ya leo tarehe 18 Agosti 2025, mahakama hiyo ilitoa amri ya kwamba inakubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam iliyoutoa Agostu 4, 2025 mwaka huu mbele ya Jaji Hussein Matembwa kukataa kurudhwa mubashara maudhui ya mashahidi wa kiraia.

Uamuzi huo ulipelekea vyombo vya Habari kushindwa kuripoti mubashara (Live) wakati Lissu akisomewa maelezo hayo ya mashahidi.

Aidha Hakimu Kiswaga alisema kuwa Shauri hilo, litakabidhiwa Mahakama Kuu kwa hatua zaidi za kisheria na atajua tarehe itakayosikilizwa kupitia Naibu Msajili wa Mahakama,

Katika kesi hiyo ya uhaini Lissu anadaiwa Aprili 3, 2025 jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam alitengeneza nia ya kushawishi au kuchochea umma ya kuweza kuzuia kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

About The Author

error: Content is protected !!