
Humphrey Polepole
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeeleza kuwa uamuzi huo wa rais, umefanyikwa chini ya mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje, imetolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Samwel Shelukindo, kupitia ilichoeleza kuwa “imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka, ikitaarifu kuwa Rais Samia ametengua uteuzi wa Balozi Hamphrey Polepole na kumuondolea hadhi ya ubalozi.”
Mbali na maamuzi hayo, taarifa hiyo, imeeleza kuwa Rais Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya utumishi wa umma, amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.
Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu tarehe 16 Julai 2025.
Balozi Polepole, alitangaza kujiuzuru akidai hawezi kuwa sehemu ya serikali isiyojali misingi ya haki, sheria na Katiba ya nchi.
Polepole amekuwa mkosoaji mkubwa wa utaratibu uliotumika kumpitisha Samia Suluhu Hassan na Balozi Emmanuel Nchimbi, kuwa wagombea wa Urais na Makamu wa Rais, katika uchaguzi mkuu unaokuja.
“Uchaguzi ule ulikiuka desturi ya CCM inayokifanya chama kuendelea kuwa imara” alisema Polepole.
Katika barua kwa Rais Samia aliyochapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Polepole alitilia doa mchakato huo na kusema, chama hicho kimenajisi mila na desturi zake.
Mbunge huyo kuteuliwa ambaye pia aliwahi kuhudumu kama balozi wa Tanzania nchini Malawi alisema, kauli maarufu ya CCM ya “Chama kwanza mtu baadaye” inafanyika vinginevyo.
“Kwa kuwa siwezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya Katiba ya nchi na chama, haki, maadili, utu na uwajibikaji wa wananchi, nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi yangu ya uongozi na utendaji serikalini,” alisema Polepole, akiongeza kuwa ataendelea kuwa mwanachama wa kawaida wa CCM.
ZINAZOFANANA
Vigogo watetea nafasi zao za ubunge ndani ya CCM
Mawakili wa Lissu wakemea manyanyaso dhidi ya mteja wao
Nani kapita, nani katemwa ubunge CCM?