
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele, ameweka wazi ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa Rais, Wabunge katika Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Akizungumza leo tarehe 26 Julai, katika viunga vya Makao Makuu ya Tume hiyo jijini Dodoma, Jaji Mwambegele amesema, tarehe 9 Agosti hadi 27 Agosti 2025, itakuwa ni kipindi cha kutoa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais.
Ameeleza pia kuwa 14 Agosti hadi 27 Agosti 2025 itakuwa ni kipindi mahususi cha utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani, huku 27 Agosti 202, ikiwa ni siku ya uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais, Makamu wa Rais, ubunge na udiwani.
Sambamba na hilo, ameongeza kuwa 28 Agosti hadi 27 Oktoba 2025, ni kipindi cha kampeni kwa Tanzania Bara na Zanzibar ili kupisha kura ya mapema.
Taarifa hii ya Tume inakiondoa moja kwa moja chama kikuu cha upinzani nchini (Chadema), katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
ZINAZOFANANA
CCM kufanya marekebisho madogo ya Katiba
Malecela atajwa kuwa mkombozi jimbo la Dodoma
Mgombea CCM agawa pikipiki kwa wajumbe