
Amos Makala
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kiweka wazi sababu ya kufanya mkutano mkuu maalumu wa chama hicho kesho kwa njia ya mtandao na kueleza kuwa ajenda ni moja tu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Ufafanuzi huo umetolewa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makala alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kwa lengo la kutoa ufafanuzi wa kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu wa CCM kwa njia ya mtandao.
Makala amesema lengo la kufanya mkutano mkuu maalunu ni kufanya marekebisho madogo ya katiba ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ameeleza kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Mapinduzi Ibara ya 99 (1) A-f (2) inaelekeza kuwa Mkutano mkuu maalumu unaweza kuhitishwa kufanya marekebisho ya katiba ya chama hicho kama kutaonekana kuna ulazima wa kufanya hivyo.
“Wanaoweza kufanya marekebisho ya katiba ya CCM ni mkutano mkuu na si vinginevyo na kwa kuwa kumeonekana kuwepo kwa ulazima ndiyo maana tunafanya mkutano mkuu kwa lengo la agenda moja tu ya kufanya marekebisho madogo ya katiba,” ameeleza Makala.
“Nimeona kwenye mitandao watu wanaulizana ni kwanini CCM wanafanya mkutano mkuu maalumu kwa njia ya mtandao, jamani kwa sasa dunia imebadilika na nilazima kwenda na Teknologia na ninawahakikishia kuwa maandalizi yako vizuri.
“Kila kitu kimeandaliwa vizuri ni wazi kuwa mkutano utafanyika vizuri na kila mtu atashuhudia kuona mkutano unavyokwwnda kwa njia ya mtandao jambo ambalo maandalizi yake yamekamilika,” ameeleza Makala.
ZINAZOFANANA
Malecela atajwa kuwa mkombozi jimbo la Dodoma
Mgombea CCM agawa pikipiki kwa wajumbe
Zanzibar yatajwa kughairishwa Kamati Kuu CCM