
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimethibitisha kuachiwa kwa Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, na Leonard Magere, Mtaalamu wa Rasilimali, Miradi na Uwekezaji, kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa na John Kitoka, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora leo tarehe 15 Julai 2025 na kusema viongozi hao wanatakiwa katika kituo kikuu cha polisi kati jijini Dar es Salaam kesho Jumatano 16 Julai 2025.
“Kila mmoja wao ametakiwa kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi kati, Dar es salaam, kesho 16 Julai 2025, kwa pamoja, Brenda na Magere walikamatwa 12 Julai 2025 katika maeneo tofauti, Magere alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (UNIA) akielekea chini Uingereza”
“Brenda alikamatwa akiwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Namanga akielekea nchini Kenya na baadaye alitegemea kusafiri kulekea nchini Ujerumani, Chadema tunaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa jambo hili na tunasisitiza haki, wazi na kufuata taratibu za kisheria katika mchakato mzima, tunaishukuru jamii ya Watanzania, Wanachama na Wapenzi wa Chadema kwa mshikamano na uungwaji mkono mnaoendelea kuonyesha katika kipindi hiki kigumu”
ZINAZOFANANA
Polepole amejiuzulu mwenyewe – Makalla
Polepole ajiuzulu Ubalozi, adai misingi ya haki imekiukwa
Maofisa wa Chadema wazuiliwa kisafiri, Polisi wasema