
MAFUNDI kuchomelea wa Mtaa wa Nyerere, kata ya Chipaka, wilaya ya Momba mkoani Songwe wametakiwa kutambua athari kubwa za kuharibu miundombinu ya serikali kwa nia ya kujipatia kipato kitendo ambacho ni kosa kisheria. Anaripoti Issa Mwadangala, Songwe … (endelea).
Kauli hiyo ilitolewa tarehe 14 Julai 2025 na Polisi kata ya Chipaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Johnson Bilingi alipokutana na mafundi hao kwa ajili ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulinda mali ya umma, hususani machuma ya madaraja na milingoti ya taa za barabarani.
Katika elimu hiyo, Mkaguzi Bilingi alieleza kuwa kitendo cha kung’oa au kuuza vifaa vya miundombinu ya serikali kinakiuka sheria za nchi na ni kitendo kinachoathiri moja kwa moja maendeleo ya jamii akiongeza kuwa serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu kwa manufaa ya wananchi wote kuiharibu ni sawa na kurudisha nyuma juhudi za maendeleo.
Ameongeza kuwa vitendo hivyo pia vinawaathiri watumiaji wa miundombinu hiyo kwani hupungua kwa usalama wa barabarani kutokana na taa kukosekana, kuvunjika kwa madaraja na kusababisha ajali ikiwemo kupotea kwa fedha za umma kutokana na marekebisho ya mara kwa mara amabayo ukwamisha shughuli za uchumi na usafiri.
Aidha, Mkaguzi Johnson Bilingi alihitimisha kwa kuwaomba wananchi wote wa kata hiyo kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha miundombinu ya serikali inalindwa kwa nguvu zote huku akisisitiza kuwa kila mwananchi ana jukumu la kufanya hivyo.
Kwa upande wao mafundi hao waliahidi kuwa mabalozi wa ulinzi wa mali za umma na walikili kuelewa elimu juu ya namna ya kutambua vifaa vilivyopatikana kiharamu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.
ZINAZOFANANA
Msikubali pombe ikasababisha kurudisha nyuma maendeleo
Polepole amejiuzulu mwenyewe – Makalla
NBC yazindua Msimu wa Pili wa Kampeni ya NBC Shambani kuhamasisha kilimo cha kahawa Ruvuma