July 14, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Polepole amejiuzulu mwenyewe – Makalla

Amos Makala

 

KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, amesema kujiuzulu kwa  aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humprey Polepole, kumetokana na utashi wake binafsi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, “Nimeisoma barua ya Polepole kupitia mitandao ya kijamia na kwamba maudhui yaliyomo ndani ya barua hiyo, ni utashi wake mwenyewe na kwamba CCM inaendelea na michakato yake kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba.”

Alikuwa akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari kufuatia barua ya Balozi Polepole, kuhusiana na yanayoendelea kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea wa ubunge na uwakilishi katika kuelekea uchaguzi ujao.

Aliongeza: “…tunaendelea na mchakato wa kupata wagombea wazuri kwa nafasi ya udiwani; wagombea wazuri kwa nafasi ya uwakilishi na wagombea wazuri kwa nafasi ya ubunge.

“Mengine sitaki kuingia ndani, ibaki ni mawazo yake, ibaki ni ridhaa yake, ni uamuzi wake, lakini amehitimisha atabaki kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi na sisi bado tunamtambua kama alivyokiri yeye mwenyewe.”

Humphrey Polepole

Polepole alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo jana Jumapili na kwamba tangu kuchukua uamuzi huo, kumeibuka mjadala kutoka kwa wachambuzi wa masuala ya kisiasa na majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii.

Baadhi yao wakienda mbali zaidi kwa kusema, kutakuwa na ugumu wa kupokelewa ndani ya chama hicho, kutokana na msimamo wake mkali.

Polepole aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Balozi wa Cuba kuanzia April mwka 2023 hadi Julai 13 mwaka 2025 alipotangaza kujiuzulu.

Barua yake ya kujiuzulu ameituma kwa rais Samia na nakala yake, ameityma ambayo nakala yake ameilekeza kwa katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kabla ya kupelekwa Cuba polepole alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, alikokutumikia kwa mwaka mmoja.

About The Author

error: Content is protected !!