July 12, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Maofisa wa Chadema wazuiliwa kisafiri, Polisi wasema

 

BRENDA Rupia Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amezuiliwa kuingia nchini Kenya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Taarifa iliyosambazwa leo tarehe 12 Julai 2025 na kusainiwa na John Kitoka Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora wa chama hicho- imeeleza kuwa Brenda aliyekuwa akisafiri kwenda nchi Kenya kwa ajili ya kikao cha masuala ya Demokrasia na Uchaguzi kinachoitangulia safari yake ya Munic- Ujerumani.

Taarifa ya Kitoka inaeleza kuwa Brenda anaendelea kushikiliwa kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga, mkoani Arusha.

Duru zinaeleza kuwa kitendo hicho kinaonesha kinawakusudia kuwadhibiti viongozi wa Chadema wasafiri nje ya nchi kwani tayari Kaimu Naibu Katibu Mkuu Amani Golugwa alizuiliwa kusafiri nje ya nchi na maofisa wa uhamiaji kwenye uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere halkadhalika na Godbless Lema alizuiliwa mpakani Namanga alipokuwa akienda Kenya kushughulikia biashara zake.

Ofisa mwingine wa Chadema, Leonard Magere, Mtaalamu wa Rasilimali, miradi na uwekezaji wa chama hicho amezuiliwa kusafiri usiku akiwa anakusudia kweda nchini Uingereza kwa ya mafunzo ya wataalamu wa kubuni mikakati ya rasilimali yaliyotarajiwa kuanza tarehe 13 mpaka 17 Julai 2025 nchini Uingereza.

John Kitoka- Mkurugenzi wa Mambo ya nje na Diaspora kipitia taarifa zake na kueleza kuwa Magere amekamatwa na kuzuiliwa kusafiri katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Leo tarehe 12 Julai 2025, viongozi hao kwa nyakataki na sehemu tofauti tofauti walizuliwa kutoka nje ya nchini.

Kwa upande wao Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa limemkamata Brenda  kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tuhuma za kutoa taarifa za uongo na za uchochezi.

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa 12 Julai 2025 na Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime imeeleza kuwa baada ya kumhoji, hatua nyingine za kisheria zitafuata kulingana na taratibu za nchi.

About The Author

error: Content is protected !!