
SERIKALI imesema kuwa inatarajia kukusanya kiasi cha Sh. 56.49 trilioni kwa ajili ya bajeti ya mwaka 2025/2026. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Akiwasilisha Bajeti hiyo Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha, amesema kuwa sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla ya Sh. 56.49 trilioni zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika mwaka 2025/26.
“Bajeti hii inatarajiwa kugharamiwa na mapato ya ndani ya sh. 40.47 trilioni, misaada sh.1.07 trilioni, na mikopo ya sh.14.95 trilioni, Kati ya mapato ya ndani yanayotarajiwa, mapato ya kodi ni sh. 32.31 trilioni, mapato yasiyo ya kodi sh. 6.48 trilioni na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Sh.1.68 trilioni.
Aidha, mikopo inajumuisha Sh. 6.27 trilioni, kutoka vyanzo vya ndani na Sh. 8.68 trilioni kutoka vyanzo vya nje,” amesema Wazari Mwigulu.
ZINAZOFANANA
TRA Mara yawaasa wananchi kuacha magendo maeneo ya mipakani
Dk Dotto Biteko kuzindua telnolojia ya kuondoa uvimbe bila upasuaji
Kesi ya Lissu yapelekwa Mahakama Kuu.