
ASKARI waliopandishwa vyeo kwa ngazi ya Sajenti na Staff Sajenti Mkoani Songwe ambao walihitimu mafunzo ya vyeo hivyo 2024/25 katika vyuo vya Polisi, Moshi, Kidatu na Zanzibar wametakiwa kuwa dira kwa wale wanaowaongoza katika usimamizi wa majukumu wanayopangiwa ili jamii iendelee kuwa salama. Anaripoti Issa Mwadangala, Songwe … (endelea).
Rai hiyo imetolewa Juni 03, 2025 na Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban baada ya kuwapokea Askari hao katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na kuwataka kutambua kuwa uongozi ni kusimamia unaowaongoza pamoja na kujua changamoto zao ili waweze kufanya kazi kwa weledi.
“Uongozi ni kusimamia Askari mnao waongoza ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano ili kuendelea kupunguza uhalifu na vitendo vya ukatili katika mkoa huu,” alisema ACP Akama.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Joseph Bukombe aliwataka Askari hao kuvitendea haki vyeo walivyovipata na kutokuwa na muhali na mtu yeyote ili kuendelea kujenga taswira nzuri ya Jeshi la Polisi kwa jamii.
Naye, Afisa Mnadhimu namba 2 wa Polisi Mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Godfrey Munguajuna alisema kuwa uongozi ni dhamana ya kuwasimamia Askari na kila cheo kinavyopanda majukumu nayo uongezeka hivyo aliwataka kuwasimamia walio chini yao ili kuleta tija ndani ya Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi limeendelea kunufaika kwa vitendea kazi na rasilimali watu katika awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo upandishwaji wa vyeo katika kada mbalimbali jambo ambalo linaongeza motisha kwa Askari na kupelekea kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii wanayoihudumia.
ZINAZOFANANA
Mahakama ya Rufaa yasisitiza Mchechu kulipwa Bili 2.5
Bei ya Petroli, Dizeli yashuka mwezi Juni
ACT Wazalendo walia kufungwa kwa Kanisa la Gwajima