
John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema
MSAJILI wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi amesisitiza ofisi yake kuwa haiwatambua viongozi saba walioteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) tarehe 22 Januari 2025 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Viongozi hao ni pamoja na John Mnyika ‘Katibu Mkuu’, Amani Golugwa ‘Naibu Katibu Mkuu – Bara’, Wakili Ali Ibrahim Juma ‘Naibu Katibu Mkuu -Zanzibar’, Godbles Lema ‘Mjumbe wa kamati kuu’, Dk. Rugemaliza Nshala ‘Mwanasheria Mkuu wa Chama’,
Wengine ni :- Rose Mayemba ‘Mjumbe wa Kamati Kuu’, Salima Kasanzu ‘Mjumbe wa Kamati Kuu’, Hafidhi Ali Saleh ‘Mjumbe wa Kamati Kuu’.
Pia Msajili amesisitiza kutowatambua viongozi na watendaji wote walioteuliwa na viongozi waliopatika kwenye Baraza Kuu pamoja watendaji au viongozi walioteuliwa kwa mamlaka za chama kushauriana na viongozi waliopatikana katika kikao cha baraza kuu la tarehe 22 Januari 2025.
ZINAZOFANANA
Dk. Mwinyi ampa heko Rais Samia ujenzi wa ofisi mpya ya CCM
Mpina ashangaa watu wanatekwa Waziri bado yupo ofisini
Mwasisi wa Chaumma atimka, asema chama kimepoteza misingi yake