May 28, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mpina ashangaa watu wanatekwa Waziri bado yupo ofisini

Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina

 

LUHAGA Mpina, Mbunge wa Kisesa (CCM), ameshangazwa na kitendo cha Waziri wa Mambo ya Ndani kuendelea kubaki ofisini wakati matukio ya watu kutekwa yameshamiri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Mpina aliyekuwa ziarani jimboni kwake leo tarehe 27 Mei 2025, amesema kitendo cha wananchi kuendelea kutoweka bila Waziri kuchukua hatua hakupaswa kuendelea kubaki ofisini.

“Mnapongezana wakati huku mtaani, watu wanatekwa, mwananchi wa kwanza, mwananchi wa pili, mpaka mwananchi 80, Waziri wa Mambo ya Ndani bado upo ofisini,” alisema Mpina na kuongeza kuwa sio kosa kisheria kwa wananchi kuikosoa serikali au kuishauri sio kosa.

“Kwa hiyo wananchi wote wanaotoa mawazo mbalimbali Tanzania kwa ajili ya kuishauri serikali, kulishauri bunge wapo sahihi na wasizuiwe na mtu yoyote.

“Hatuwezi kuzimaliza changamoto za taifa letu kwa kuongea kwa lelemama, kwa kutoambizana ukweli hata mahala palipoharibika mnapongezana watu wanatekwa nyinyi,” amesema Mpina.

Mpina amesema kuwa atadumisha utamaduni wake wa kupigania haki bila woga na kwamba hakuna mipaka ya kukosoa viongozi wa umma.

“Mimi kijana wenu ni mkweli sana na nataka niwahakikishie tutaendelea kuwapigania bila uwoga mahala popote tutaendelea kuyasongesha maendeleo ya Tanzania, tutaendelea kumsimami kiongozi yoyote yule Tanzania bila kuogoa wakati wowote na mimi msimamo wangu viongozi yoyote wanakosolewa kila kiongozi hawezi kuwa na kinga ya kukosolewa Diwani, Mbunge na Rais anakosolewa lakini wanapofanya vizuri wapongezwa,” alisema Mpina.

About The Author

error: Content is protected !!