
SALUM Mwalimu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), amesema kuanzia tarehe 30 Mei 2025, jijini Mwanza watazindua rasmi Oparesheni ya ‘C4C’ itakayozunguka nchi nzima kwa siku 16. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Ameyasema hayo leo Mei 21,2025 kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapokea wanachama wapya wa CHAUMMA kutoka vyama mbalimbali.
Amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupeleka neno la matumaini kwa watanzania na kuwaambia wasiwe na hofu sauti zao bado zinasikika na kuwa wapo waliotayari kuzibeba sauti hizo kwa gharama yoyote na kuwaomba wajiandae.
Kiongozi huyo amesema kuwa ratiba kamili ya ziara hiyo nchi nzima, itatoka hivi karibuni na watatumia usafiri wa chopa katika kuwafikia wananchi.
Pia amesema Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa CHAUMMA atawatangazia ratiba ili wanachama waanze maandalizi ya vikao na mikutano kwenye majimbo yao.
ZINAZOFANANA
Mvunde aongoza kikao cha kimkakati wa kiuchumi kupitia STAMICO
CBE yajivunia mchango wa wahitimu wake
MERIDIANBET yagusa mioyo ya watu, yafika Makumbusho, M’nyamala kutoa msaada familia zenye mahitaji