HATIMAYE yametimia, Gazeti la MwanaHALISI toleo Na.507 la tarehe 8 -14 Mei 2025 lilifichua kuwa kundi la G55 litajiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) hatimaye leo tarehe 19 Mei kundi hilo limejiunga na chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mwenyekiti wa chama hicho Hashimu Rungwe amewapokea wanasiasa hao waliovuna vyeo katika chama hicho.
Kamati Kuu ya Chama hicho ilizijaza nafasi zilizokuwa wazi katika chama hicho ambazo ni pamoja na Katibu Mkuu ambayo ameteuliwa Salum Mwalimu, Devotha Minja akikaimu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara na Benson Kigaila akikaimu nafasi ya Naibu katibu Mkuu Bara.
ZINAZOFANANA
Tanzania yaibuka kinara wa utalii duniani
TRA yawataka wanachama wa SACCOS kuhamasisha ulipaji kodi
Mwanasheria wa kimataifa ataka Tanzania isifukuzwe Jumuiya ya Madola