
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeusisitiza upande wa Jamhuri kwenye kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kukamilisha upelelezi wa shauri hilo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Awali upande wa Jamhuri ulidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo unaendelea chini ya Jeshi la Polisi na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Jopo la Mawakili wa utetezi liliongozwa na Wakili Dk. Rugemaliza Nshala, Mpale Mpoki, Peter Kibatala, lilipinga kauli hiyo ya upande wa Jamhuri na kuimba mahakama kuitaka upande huo useme kinachokwamisha upelelezi huo.
Upande wa utetezi ulieleza mahakamani hapo kuwa mteja wao (Tundu Lissu) hajakutwa na hatia hivyo wameiomba mahakama hiyo kuondoa ulinzi wa askari hao unaopelekea kupunguza uhuru wa mteja wao mahakamni na kwamba kitendo hicho ni kinyume na katiba.
Katika hatua nyingine upande wa utetezi umeiomba mahakama hiyo, kutosikiliza shauri kwa njia ya mtandao kwa ilivyoamuriwa kwenye kesi ya uchochezi.
Upande wa Jamhuri ulieleza kuwa hoja ya utetezi haina mashiko na kwamba ulinzi huo unatija kwa mtuhumiwa.
Upande wa Jamhuri ukijibu hoja za ucheleweshwaji wa upelelezi huo, umedai kuwa hakuna sheria yoyote inayowalazimisha kueleza suala la upepelezi.
Baada ya mabishano makali kisheria Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Franco Kiswaga amesema kwa kuwa shauri hilo linagusa hisia za wengi hoja za upande wa utetezi, zina mashiko na kwamba shauri hilo litatajwa terehe 2 Juni 2025, na Lissu atafikishwa mahakamani hapo.
ZINAZOFANANA
Salum Mwalimu Katibu Mkuu mpya Chauma
Serikali kufikisha mashahidi 15 kumkabili Lissu kizimbani
DC Arusha aongoza matembezi ya Rotary Walk & Run kuchagia damu