May 19, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

DC Arusha aongoza matembezi ya Rotary Walk & Run kuchagia damu

JOSEPH Mkude, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, kwa niaba ya Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Arusha ameongoza mamia ya wananchi na wadau mbalimbali katika matembezi ya hisani ya Rotary Walk and Run yaliyofanyika Jana katika viwanja vya Gymkhana, jijini Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Matembezi hayo yameandaliwa kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji wa damu salama pamoja na kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa jengo la benki ya damu linaloendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha – Mount Meru.

Akizungumza baada ya matembezi hayo, Mkude amewapongeza waandaaji wa tukio hilo kwa kuonesha moyo wa uzalendo na kujali maisha ya watanzania, huku akisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji msaada wa haraka hospitalini.

“Uchangiaji wa damu salama ni suala la msingi kwa ustawi wa afya ya jamii. Kupitia tukio hili, tunapata fursa ya kushiriki moja kwa moja katika kuokoa maisha. Pia, tunasaidia kupunguza changamoto za upatikanaji wa damu hospitalini,” amesema. Mkude.

Kwa upande wao, waandaaji wa matembezi hayo kwa kushirikiana na mashirika ya kijamii na wafadhili mbalimbali, wameeleza kuwa fedha zitakazokusanywa zitapelekwa moja kwa moja katika ujenzi wa jengo jipya la benki ya damu ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi na kusambaza damu salama kwa wahitaji.

About The Author

error: Content is protected !!