
JUMAA Aweso, Waziri wa Maji amewataka wataalamu wa mabonde kujikita katika kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi ili huduma ya maji kwa wananchi iwe endelevu. Anaripoti Joyce Ndeki, Dodoma … (endelea).
Aweso ameyasema hayo leo Mei 9, 2025 wakati akikabidhi vifaa vya kisasa vya utafiti wa maji chini ya ardhi vilivyonunuliwa kwa fedha za UVIKO.
“Vifaa hivi viwe chachu ya kuwaongezea uwezo wataalamu wetu na kuweka nguvu katika utafiti ili maeneo yaliyokuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji yapate maji,” amesema Waziri Aweso na kuongeza kuwa vifaa hivyo vinagawanywa katika mabonde tisa ya maji.
George Lugomela, Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za Maji, amesema vifaa hivyo vitawezesha kuchunguza uwepo wa miamba inayohifadhi maji kwa ufanisi hadi kina cha urefu wa mita 1000.
Vifaa hivyo ni pamoja na cha kuchunguza mipasuko katika miamba kwa njia ya sumaku (magnetrometer), kifaa cha kuchunguza maji (terrameter), kifaa cha kupima kina cha maji (deeper),kifaa cha kuchunguza mikondo ya maji na kifaa cha kuchukua majira (GPS).
Lugomela amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha kwa fedha zinazosaidia kufikisha azma ya kupata huduma ya maji kwa wananchi kwa asilimia 85 vijijini na 95 mjini ifikapo 2025.
ZINAZOFANANA
Serikali kuongeza thamani ya madini
Kadinali Robert Prevost atangazwa kuwa Papa mpya
Chatanda ashuhudia utiaji saini wa Bil 13.3 kuboresha miundombinu Rufiji