
Rais Samia Suluhu Hassan
DK. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameongeza mshahara kwa wafanyakazi wa Umma wenye kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 35.1 na nyongeza hiyo itaanza kufanya kazi mwezi Julai mwaka huu. Anaripoti Joyce Ndeki, Singida … (endelea).
Amesema hayo leo tarehe 1 Mei 2025, kwenye maadhimisho ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika mkoani Singida na kusema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo maslahi ya wafanyakazi kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu.
Pia Dk. Samia ametoa onyo kwa vyama vya wafanyakazi kwa kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma na kusimamia kikamilifu maslahi ya wanachama.
Hata hivyo amesema Serikali imepokea ushauri wa Chama cha Wafanyakazi Tanzania (Tukta), wa kusimamia kwa ukaribu ajira za mda mfupi ili kuhakikisha zinazingatia viwango vya ajira zenye staha wanazostahiki kwenye ajira zao na kuzitaka wizara husika kusimamia hilo.
Amesema serikali inaendelea kushirikisha wadau na makundi mbalimbali ya wananchi kufanya utambuzi wa kaya zisizo na uwezo ili kuboresho mifumo ya utoaji wa huduma na kuandaa vitita vya mafao vitakavyokuwa nafuu kwa gharama na kuwasihii wastafu kujiunga na bima ya afya.
Rais Samia amesema serikali imeongeza ukuaji wa uchumi kwa asilimia 5% kutoka 4.6% ya mwaka 2023 na wamefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei kutokana na uwekezaji na uzalishaji na mauzo ya nje na kujenga mazingira mazuri kisera na kisheria.
ZINAZOFANANA
Padre Kitima amuibua Mbatia
Luhemeja ataka Afrika yenye kukabili mabadiliko ya tabianchi
Mtu mmoja mbaroni kwa kushambuliwa Padri Kitima