
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkunguni Kariakoo Jijini Dar es Salaam muda huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Heche amekamatwa na Polisi baada ya jeshi hilo hilo Wilaya ya Kariakoo kukiandikia barua ya chama hicho kuzuia mkutano huo.
Barua hiyo iliyowataka Chadema kutofanya mkutano huo uliopangwa kufanyika katika mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni kwa sababu ya shughuli za biashara zinazoendelea eneo hilo.
Duh!
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, “kukosoa na kukosoana, ni silaha za mapinduzi.”
Iweje leo polisi wanatumiwa kuzuia hayo.
Je, kuna mfanyabiashara aliyepeleka malalamiko yake polisi?
Je, sheria ya mikutano inasema lazima ifanyike kwenye viwanja?
Ni lini polisi wa Afrika wakaacha siasa na kujikita kwenye uhalifu?
Kusulubu wapinzani ni udhaifu wa CCM.