April 15, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

NIDA kusitisha namba ya utambulisho Mei Mosi

 

MKURUGENZI wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), James Kijo, ametangaza kuanzia tarehe 01 May, 2025 NIDA itasitisha rasmi matumizi ya Namba ya Utambulisho wa Taifa (NINs) kwa wote ambao walitumiwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) lakini hawakujitokeza kuchukua vitambulisho vyao. Anaripoti. Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema hayo tarehe 14 Aprili 2025 katika mkutano na waadishi wa habari, ameeleza kwamba yule ambaye matumizi ya namba yake ya NIDA yatafungwa hatoweza kuitumia namba hiyo kwa ajili ya huduma yeyote.

Kaji amesema, dhamira yao na Serikali kwa ujumla ni kuona kila Mtanzania anapata kujulikana na kufikiwa na huduma za msingi zikihitajika na kila kitambulisho kilichotengenezwa kinachukuliwa na Mhusika na hasa ikizingatiwa Serikali imetumia fedha nyingi kutengeneza.

Amefafanua ”tangu kuanza kwa zoezi hilo mwezi Januari hadi kufikia Machi mwaka huu jumla ya Wananchi 1,88608 sawa na asilimia 157 ya Watu wote walikuwa hawajachukua vitambulisho vyao licha ya kutumiwa ujumbe mfupi (sms).

“Kwa mujibu wa takwimu hizi idadi ya vitambulisho 1.2 milioni vilikuwa havijachukuliwa na wahusika ilhali walikuwa wamepata ujumbe kupitia simu zao za mikononi, aidha wananchi waliojitokeza kuchukua vitambulisho baada ya kupokea sms ni 565,876 sawa na asilimia 30 tu ya Watu wote waliotumiwa na kupokea sms”

Aidha , Kijo amesema kuanzua mwezi July mwaka huu Mamlaka hiyo  imeaandaa mpango wa usajili na utambuzi wa Watu wote wenye umri kuanzia 0 hadi miaka 18 ili kuwezesha upatikanaji wa Jamii Namba pamoja na wageni wote wanaoingia nchini na kukaa chini ya miezi sita.

Mwisho ametoa rai kwa wananchi wote kuhakikisha kuwa wanakuwa na vitambulisho vyao kwasababu mamlaka hiyo inakwenda kufanya maboresho ya kuongeza matumizi mengine kama passport, leseni za udereva pamoja na usajili wa mambo mengine mengi.

About The Author

error: Content is protected !!