
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wassira
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amesema deni lililopo la Sh. 97 trilioni sio kwamba lote limekopwa na Rais Samia bali limekuwepo tangu enzi za Rais wa kwanza, Hayati Mwalimu Julius Nyerere. Anaripoti Mwandishi Wetu. Simiyu … (endelea).
Ameyasema hayo leo 29 Machi 2025 wakati akizungumza na wanachama pamoja na viongozi wa CCM Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu katika kikao cha ndani kikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo, yenye lengo la kukagua uhai wa Chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kusikiliza kero za wananchi.
Amesema nchi inakopa kwa ajili ya kufanya mambo tukayoishi nayo na faida zake zitakuwepo kwa miaka mingi kwa kizazi cha sasa na hata kijacho.
“Tunakopa ili kufanya jambo ambalo tutaishi nalo na faida zake kwa miaka mingi kizazi hiki na hata kizazi kijacho na lile deni sio kwamba amekopa Rais Samia trilioni 97 sio kweli, lile deni linaongezeka na madeni mengine ya zamani ambayo tulishakopa tangu enzi za Nyerere, alichukua miaka 40 kuanza kulipa nayo yamo katika hesabu,” amesema Wassira.
Acha kutuzuga. Mikopo imepaa mno chini ya Mama!