
KATIBU Mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilbroad Slaa amewataka watanzania kuacha kudanganyika na propaganda za kitoto kuhusu kuhusishwa kwake kurejea CHADEMA ili kuwa mgombea urais. Anaripoti Apaikunda Mosha, Mbeya … (endelea).
Slaa ameyasema hayo hii leo tarehe 24 Machi 2025, wakati akiwa ameambatana na makamu mwenyekiti wa chama hicho Bara John Heche, kwenye mahojiano na Kyela Fm, jijini Mbeya.
Katika mazungumzo yake Slaa amesema kwa umri wake sasa wa miaka 76 hakuna ambacho anakitafuta, isipokuwa kujenga maisha na maslai ya vijana wenye nias njema na nchi hii ambao amewatumikia kipindi cha miaka yote.
Alisema ”Nimekuwa kwenye utumishi sehemu mbalimbali nilizopita kwa miaka zaidi ya 30, CHADEMA tu nimeka zaidi ya miaka 20, leo mtu anakuja na propaganda nyepesi, hizo ni za kupuuza, tunahitaji vijana mtu kama heche akigombea urais leo, hawezi kuikoa Tanzania?,”
Aliongeza “Kwanini tunamfikiria Slaa ambaye amefikia mwisho wake, yeye kazi yake ya sasa ni kusaidia wajukuu zake, nimerudi kwa sababu nina uchungu, serikali tuliyonayo imeshindwa kwa kuangamiza yale yote ambayo Mwalimu aliyaweka kwa ajili ya utajiri wa Taifa hili.”
“Nimerudi sasa ili nisaidiane wakina Heche, Lissu na vijana wengine wa CHADEMA ambao wanania njema na nchi hii, tuna muhitaji Mussa nchi hii, wakulitoa taifa hili liende kwenye nchi ya raha, asali na maziwa na uwezekano huo tunao,” amesisitiza Slaa.
Aidha, viongozi hao wanatarajia kufanya mikutano ya hadhara kwenye majimbo ya Kyela, Busokelo na Rungwe, katika muendelezo wa kampeni ya ‘Hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi’ (‘No Reforms, No Election’).
ZINAZOFANANA
Hatua za msajili analenga kuinyamazisha ajenda ya Chadema
Askofu Mwamalanga akemea vikali kauli ya Makala
Tundu Lissu atoa sababu za kutaka mabadiliko ya Uchaguzi