
Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema chama kimekubaliana kuwepo mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi ili uchaguzi usimamiwe na watu waliohuru na sio waajiriwa wa serialikali wala kutoka chama chochote cha siasa. Anariopoti Mwandishi Wetu, Rukwa … (endelea).
Akihutubia katika mkutano wa hadhara Kabwe, Rukwa leo tarehe 24 Machi 2025, Lissu amewaeleza wananchi hao mambo yaliyokuwa yakifanyika katika chaguzi zilizopita.
Lissu alisema “Hebu fikiria ni kitu gani kilichofanya CHADEMA itoke wabunge 72 mwaka 2015 mpaka abaki Aida pekee ake, ni kitu gani tulichowakosea watanzania mpaka watukatae namna hiyo?”
Aliongeza kuwa, “watanzania hawakutukataa kilichotokea ni kwamba, CCM iliwaamuru wasimamizi wake wa uchaguzi, Wakurugenzi wa Halmashauri.. wanaotangaza matokeo wakaambiwa ole yake atakayetangaza mpinzani ameshinda ubunge, ndio maana nchi nzima aliyetangazwa kwa nguvu kubwa ya wananchi ni Aida pekee yake.”
Amesema kazi iliyopo sasa hivi kuelekea uchaguzi ni kuhakikisha mfumo wa uchaguzi unabadilishwa ili wakurugenzi wa halmashauri ya CCM wasiwe wanatangaza tena matokeo ya uchaguzi.
“Hatutaki tena utendaji ambao watendaji wa kata ni wanaCCM, Waalimu na Manesi hatutaki tena wasimamie uchaguzi kwenye vituo vyetu vya kupigia na kuhesabia kura,” amesema Lissu.
ZINAZOFANANA
Hatua za msajili analenga kuinyamazisha ajenda ya Chadema
Askofu Mwamalanga akemea vikali kauli ya Makala
Slaa: Watanzania msidanganyike na propaganda za kitoto