
Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
WAZIRI wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amemkemea vikali, ruhusa iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila katika kipindi cha muda mfupi, kuruhusu magari ya kawaida kupita kwenye baadhi ya Barabara za Mwendokasi ikiwemo ya Mbagala, kwa sababu hawakuwa na mamlaka hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mchengerwa amesema hayo hii leo tarehe 21 Machi 2025, wakati wa tukio la utiaji saini mradi wa DMDP Awamu ya pili, katika mikataba ambayo itahusisha ujenzi wa Barabara katika Halmashauri tano za Dar ea Salaam.
Waziri huyo aliendelea kusema kuwa, kitendo cha kuruhu magari ya kawaida kupita, kimesababisha barabara ya mwendokasi Mbagala kuanza kuharibika, kabla ya magari husika kuanza kupita.

“Mlitoa maelekezo wakati fulani ya kuruhusu magari kupita katika barabara za mwendokasi, mkasahau ya kwamba barabara za mwendokasi sio za kwenu ni za Waziri wa Tamisemi, nyinyi mkaruhusu watu wakapita wakati ule, nimewasamehe.
“Lakini maelekezo yangu, barabara ya mwendokasi Mbagala yamapita Malori ya tani 30 mpaka tani 40, barabara imeanza kuharibika madhara yake miradi hii itakwenda kusimama,” alisema Mchengerwa.
Pamoja na hayo Waziri huyo ametoa maelekezo ya kutoruhusu, magari ya kawaida kupita wenye Barabara hizo za Mwendokasi, ili kuitunza miundombni hiyo iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.
ZINAZOFANANA
Wanafunzi wahimizwa kulinda miundombinu ya shule
NIT yajivunia uanzishwaji wa chuo cha marubani
Asilimia 11 tu ya wanawake wamenufaika na TIB