March 18, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

NSSF kutoa mafao siku moja baada ya mwanachama kustaafu

 

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF umesema umejipanga kutoa mafao kwa mstaafu siku moja baada ya kupewa barua yake ya kustaafu badala ya kusubili kulipwa mafao yake kwa siku 60 tangu kustaafu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Masha Mashomba, alipokuwa akitoa taarifa kwa Umma kwa waandishi wa habari juu ya mafanikio.ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka 4 katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari -MAELEZO Jijini Dodoma.

Mashomba amesema hatua hiyo inatokana juhudi na umakini wa mfuko kwa kuhakikisha wastaafu ambao ni wachangiaji wa kuu wa mfuko huo wanapostaafu wasipate shida au kuchukua muda mrefu kupata mafao kwa muda mfupi badala ya kuchukua muda mrefu.

Hata hivyo amesema kuwa kwa sasa NSSF inatoa mafao kwa wastaafu ndani ya siku 30 tangu mstaafu anapokuwa amestaafu tofauti na ilivyo mifuko mingine.

Aidha ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka mnne NSSF imejinasibu kwa kupata mafanikio kwa asilimia 92 sambamba na kuongeza wanachama lukuki.

Mashomba amesema kuwa mafanikio hayo hadi kufikia asilimia 92 ni juhudi za Serikali pamoja na kuwa na mashirikiano mema ya watumishi wa mfuko huo pamoja na kuongeza wanachama wapya wanaochangia mapato ya mfuko huo.

Mafanikio hayo yanaendana na mwenendo Mzuri wa ukuaji wa Mfuko ukichangiwa na ongezeko la asilimia 92 katika thamani ya Mfuko Katika kipindi husika, thamani ya Mfuko imeongezeka kwa asilimia 92 kutoka Sh. 4.8 bilioni mwezi Februari 2021 hadi kufikia Sh. 9.2 bilioni mwezi Februari 2025.

Amesema kuwa ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa wanachama, mapato yatokanayo na michango na kukua kwa thamani ya vitegauchumi vya Mfuko.

“Mwenendo mzuri wa ukuaji wa Mfuko unaashiria uhimilvu na uendelevu imara wa Mfuko ya wanachama Wanachama wapya 1,052,176 wameandikishwa Katika kipindi cha miaka minne kilichoanzia Machi 2021 mpaka Februari 2025, Serikali ya Awamu ya Sita imetekeleza mikakakati mbalimbali katika kuimarisha uchumi na kufungua fursa za uwekezaji na biashara.

“Katika kipindi husika, Mfuko umeandikisha jumla ya wanachama wapya 1,052,176. Matokeo ya jitihada hizo yamekuwa na matokeo chanya katika ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara, kilimo, utalii na miundombinu.

“Utekelezaji wa miradi mkubwa kama vile ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere; Mgodi wa Nyanzaga,Kiwanda cha mbolea Intracom,Kiwanda cha vifaa vya umeme cha Elsewed Electric East Africa Ltd; Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato; Mgodi wa Uchimbaji wa Madini ya Nikeli (Tembo) uliopo Ngara; Daraja la Kigongo-Busisi Mwanza ,kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo na Mkulazi Morogoro na mradi wa reli ya kisasa ya SGR, umechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la wanachama na michango inayochangia katika ukuaji wa Mfuko.

“Michango ya Sh. 6.9 bilioni imekusanywa Katika kipindi husika, Mfuko umeongeza uwezo wake wa kukusanya michango ambapo jumla ya Sh. 6.9 bilioni zimekusanywa kutoka kwa wanachama na michango ya inayokusanywa kwa mwaka ikiongezeka kutoka TZS bilioni 1,131.92 katika mwaka ulioishia Februari 2021 hadi kufikia Sh. 2.1 bilioni katika kipindi kilichoishia Februari 2025 sawa na ongezeko la asilimia 90. 3.

“Thamani ya vitega uchumi vya Mfuko (Investment portfolio) imeongezeka kwa asilimia 92,katika kipindi husika, thamani ya vitega uchumi vya Mfuko (investment portfolio) imeongezeka kutoka TZS bilioni 4,283.32 katika mwaka ulioishia Februari 2021 hadi kufikia TZS bilioni 8,212.92 katika mwaka ulioishia Februari 2025 sawa na ongezeko la asilimia 92.

” Ustahimilivu wa Mfuko (funding level) kutokana na tathmini ya uhai na uendelevu wa Mfuko imefikia asilimia 90.7 Matokeo ya tathmini ya uhai na uendelevu wa Mfuko katika kipindi kinachoishia mwezi Juni 2023 yameonesha kuwa, kiwango cha sasa cha uchangiaji (contribution rate) cha asilimia 20 kitatosha kugharamia ulipaji wa mafao, gharama za uendeshaji pamoja na gharama zingine kwa kipindi kirefu,” ameelezea Mkurugenzi.

Akiendela kuelezea mafanikio.amesema kuwa tathmini inaonesha hali ya ustahimilivu ya Mfuko (funding level) ni asilimia 90.7 kwa kipindi kilichoishia Mwezi Juni 2023 ukilinganisha na asilimia 87.7 iliyokuwepo katika tathmini ya kipindi kilichoishia mwezi Juni 2020.

About The Author

error: Content is protected !!