March 17, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Bil 3.4 zatumika kulipa fidia wamiliki wa ardhi Dodoma

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema serikali imetoa Sh. 3.4 bilioni kwa ajili ya kulipa fidia wananchi ambao walipisha miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa kwenye ardhi walizokuwa wanazimiliki. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dodoma … (endelea).

Ameyasema hayo Jumatatu 17 Machi 2025, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Sera ya Taifa ya ardhi ya mwaka 1995 toleo la 2023, pamoja na hayo ameishukuru wizara hiyo kwa uzinduzi wa sera hiyo ambayo itasaidia kupunguza kero nyingi na kuongeza kasi ya utoaji wa hati.

Vilevile Senyamule ameipongeza serikali kwa uwekezaji mkubwa na maboresho  yaliofanyika jijini hapo jambo ambalo linafanya thamani ya ardhi ya jiji hilo inaendelea kuongezeka kutokana uhitaji mkubwa wa ardhi kutoka kwa watu mbalimbali.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa uhitaji huu wa ardhi hasa kwa jiji la Dodoma umepelekea kuibuka kwa migogoro mingi ya ardhi aidha, na hivo Rais Samia alitoa wito  kutatua kero hizo ili wananchi wakae kwa Amani na utulivu na hivi sasa kazi inaendelea kufanyika na kwa utashi mkubwa ya kutatua migogoro hiyo.

“Kwa kipindi cha miaka minne kero zaidi ya 24,000 zinazohusu ardhi zimeweza kutatuliwa katika  Mkoa wetu wa Dodoma zikiwemo kero za madai ya fidia, mahitaji ya viwanja, ucheleweshaji wa hati, milki pandikizi na mambo mengine,” amesema Senyamule.

Aidha, kati ya madai 3200 ya madai ya viwanja vilivokuwa vinataka mbadala, viwanja 1215 vimeshatolewa na 1337 vinatarajiwa kutolewa kabla ya kuisha mwezi april, jambo ambalo litapunguza deni hadi kufikia 1216 ambavyo vinataftiwa utaratibu wa  kukamilishwa kwake.

About The Author

error: Content is protected !!