
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa Bwawa la maji, Kidunda mkoani Morogoro, mradi huo umefikia 28% utakapokamilika unatarajia kuboresha huduma ya Majisafi kwa ajili ya matumizi ya Majumbani, Kilimo, uvuvi na Viwanda. Anaripoti Apaikunda Mosha, Morogoro … (endelea).
Baada ya tukio hilo lililofanyika katika wiki ya maadhimisho ya maji leo tarehe 5 Machi 2025, ameeleza kuwa mradi huo ni fursa kwani unakwenda kutengeneza ajira nyingi kwa wananchi wa Ngerengere.
Amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kuwa na mtambo wa uzalishaji umeme megawati 20, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye urefu wa kilomita 101 kutoka Kidunda hadi Chalinze kwenye gridi ya Taifa pamoja na ujenzi wa barabara kiwango cha Changarawe yenye urefu wa kilomita 75 kutoka Ngerengere hadi Kidunda
Majaliwa amesema utekelezwaji wa mradi huu ni takribani Tsh. 336 bilioni, hivyo amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji aidha, mradi huo utakuwa wa kudumu pale ambapo vyanzo vya maji kutoka mto Ruvu vitakuwa vinatiririsha maji yake kama inavotakiwa hivyo lazima kuvitunza na kuvihifadhi vyema.
Pamoja na hayo Bwawa hilo lina uwezo wa kuhifadhi maji lita 190 bilioni, hivyo litanufaisha tarafa nzima ya Ngerengere, wanachotakiwa ni kuvitambua na kuvilinda vyanzo vya maji hayo, amesema wapo wananchi wanakiuka sheria za utunzaji wa mazingira, aidha kwa mwaka 2021/22 kulitokea ukame kutokana na ukataji wa miti ovyo na uharibifu wa vyanzo vya maji, hivyo serikali itachukua hatua kwa watu hao kwa kuwa nia yao si njema.
“Tumekuwa tukipata shida ya upungufu wa maji kwenye maeneo ya miji, haya yametokana na ukosefu wa maji kwenye vyanzo vya maji, leo tuna kilio cha kutopatikana maji vijijini unadhani serikali haileti maji? amesisitiza kuwa fedha ya kuleta maji ipo lakini maeneo ya kuleta maji hayapo kwa sababu tumeyaharibu, tumeyakausha kwa shughuli zisizofaa,” amesema Majaliwa.
Aidha, ameitaka kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wananchi kulinda vifaa vyote vinavyotumika katika ujenzi wa mradi huo (mafuta ya mitambi, saruji, nondo, vifaa vya umeme) ili kuhakikisha hakuna tatizo la kuibiwa au kupotea kwa vifaa vya ujenzi.
ZINAZOFANANA
Puma Energy Tanzania yazindua awamu ya pili ya Kampeni ya Usalama Barabarani kwa wanafunzi wa msingi
Waziri Mkuu Majaliwa aonyesha maendeleo katika huduma ya Afya
Marvel Gold kuanzisha mgodi wa dhahabu Hanang