
KATIKA kipindi cha miaka minne ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imepokea jumla ya shilingi Bilioni 56.24 kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya elimu Tanzania. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hayo yameelezwa na Erasmus Kipesha alipokuwa akitoa taarifa na utekelezaji na maendeleo katika mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasani aliyoitoa kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari Maelezo Jijini Dodoma.
Akitoa ufafanuzi zaidi Kipesha amesema kuwa Mamlaka hiyo imepokea kiasi cha Sh. 49.05 bilioni kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya Mfuko wa Elimu na jumla ya Sh. 3.8 bilioni kwa ajili ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi.
Ameeleza kuwa katika kipindi hicho hicho Mamlaka imepokea jumla ya shilingi Bilioni 4.11 kutoka kwa wadau kuwezesha utekelezaji wa miradi kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa. Vile vile, wadau wametoa michango ya vifaa vyenye thamani ya Sh. 269.3 milioni.
Aidha ameeleza kuwa Kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA, katika kipindi cha miaka minne 2021/2022 hadi 2024/25, Sh. 49.05 bilioni zimegharamia ufadhili wa miradi 3,768 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika maeneo mbalimbali nchini.
ZINAZOFANANA
Dk. Biteko awapongeza Exim kuzindua tawi Kahama
ITC watakiwa kuwajengea uwezo wakulima na wafugaji nchini
Benki ya Exim yaingia mkataba wa miaka mitatu na ZATI