
CHAMA cha ACT Wazalendo kinatarajia kufanya kikao cha Halmashauri Kuu siku ya tarehe 23 Februari, 2025 jijini Dar es Salaam. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa iliyotolewa tarehe 21 Februari 2025 na Naibu Katibu wa idara ya habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa Chama cha ACT Wazalendo, Shangwe Ayo, inasema kikao hicho kitafanyika makao makuu ya chama, katika ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo jengo la Maalim Seif, Magomeni Dar es salaam.
Aidha, kikao hicho cha Halmashauri Kuu kitatanguliwa na Kamati Kuu ambayo itakutana tarehe 22 Februari, 2025 Makao Makuu ya Chama.
Taarifa hiyo ilieleza, Halmashauri Kuu inatarajia kupokea taarifa ya kina ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024. Hivyo wajumbe watafanya tathmini kwa kina kuhusu chaguzi huo na kutoa maagizo kwa Chama juu ya hatua muafaka za kuchukua.
Pamoja na hayo Halmashauri Kuu, itajadili na kutoa mwelekeo wa Chama kuelekea uchaguzi mkuu wa unaotarajia kufanyika mwaka 2025.
Aidha taarifa inaeleza kuwa kwa halmashauri Kuu hicho ni kikao cha pili kwa ukubwa na kimadaraka cha ACT Wazalendo, baada ya Mkutano Mkuu.
ZINAZOFANANA
Samia: Uhitaji wa kahawa duniani ni fursa kwa Afrika
Shigongo: Tutumie rasilimali zetu kuzibadilisha kuwa fedha
Dk. Nchimbi awatangazia kiama wanaosaka uongozi kwa kuchafuana na matamko