
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama
KAIMU Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa jitihada kubwa ambazo zimefanyika katika huduma ya maji Wilaya ya Kinondoni. Anaripoti Apaikunda Mosha. Dar es Salaam … (endelea).
Amezungumza haya katika Kikao Kazi cha DAWASA kilichofanyika leo tarehe 18 Februari 2025, amesema Kinondoni ina kata 20 na mitaa 106, lakini DAWASA imefika kwenye mitaa yote kwa kiwango tofauti na bado kazi inaendelea baadhi ya mitaa.
“Kinondoni ipo wastani 95% wa kazi ya maji imefanyika na bado kazi inaendelea kufanyika,” Mhandisi Bwire ameeleza kuwa mpaka sasa usambazaji wa maji kwa jiji la Dar es Salaam umefikia wastani wa asilimia 93 huku kwa Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni asilimia 97.
“Ni kazi ya DAWASA na wenyeviti wa mitaa kuhakikisha wanawashawishi watu kujiunga na huduma ya maji ambayo Serikali imefanya kazi yake kwa asilimia 97 ya kupeleka mitandao ya mabomba katika maeneo ya makazi ya watu,” amesema Mhandisi Bwire.
Aidha amesema kuwa wenyekiti wa vijiji waanze kufanya tathmini ya kaya na nyumba katika maeneo yao ili waweze kujua upatikanaji wa maji kwenye kaya zao na kuhakikisha watu wapate maji safi na salama ili kuepuka matatizo ya magonjwa na kulinda Afya za watu.
ZINAZOFANANA
SBL yazindua kampeni ya SMASHED kukabiliana na unywaji wa pombe chini ya umri
DAWASA wajitia kitanzi changamoto za maji Temeke
Uingereza yafurahishwa na maboresho Bandari ya Dar, yaipongeza serikali