
Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu (TANROAD), Mhandisi Ephatar Mlavi
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji mkuu wa Serikari, Greyson Msigwa, amewataka wakuu wote wa Taasisi za Serikali kuhakikisha wanatoa taarifa zao za utekelezaji wa shughuli za maaendeleo kwa Umma kupitia vyombo vya habari kwa miaka 4 ya uongozi wa Rais wa awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasani. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Msigwa ametoa maagizo hayo leo Jumatatu tarehe 17 Februari 2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari Maelezo Jijini hapa wakati wa kipindi cha utoaji wa taarifa ya maendeleo kwa miaka 4 ya Wakala ya Barabara Tanzania (TANROAD).
Wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu (TANROAD), Mhandisi Ephatar Mlavi, Msigwa amesema ni wajibu wa kila Taasisi ya Serikali kuhakikisha inatoa mawasilisho ya taarifa ya maendeleo kadri walivyopangiwa tarehe za kuwasilisha taarifa hizo.
“Hapa naongea kama katibu mkuu nawaagiza viongozi wote wa taasisi za serikali kuhakikisha zinafanya mawasisho ya taarifa za maendeleo kwa kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais wa awamu ya sita.
“Ikitokea kiongozi wa taasisi hakawa hajawasilisha taarifa ya maendeleo kwa taarifa aliyopangiwa bila kutoa taarifa ya msingi itabidi aandike barua ya kujieleza ni kwanini hajafuata utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa,” ameeleza Msigwa.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Wakala ya Mipango ya Miundombinu (TANROAD) Ephatar Mlavi amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais wa awamu ya 4 umekuwa na mafanikio kwa asilimia 90 ikilinganishwa na asilimia 86 Julai 2021.
Idha Mlavi amesema kuwa Serikali imefanikisha kujenga mtandao kwa barabara za lami,madaraja na viwanja vya ndege ambavyo vipo kwa hali mzuri.
Amesema Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita kuanzia mwaka 2021 hadi Februari 2025, Serikali imepata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege nchini.
Ameeleza kuwa Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 15,625.55 zimekuwa katika hatua mabalimbali za utekelezaji ambapo barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 1,365.87 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 2,031.11 zimeendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.
“Aidha, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 2,052.94 na madaraja mawili (2) zimefanyiwa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina na Serikali inatafuta fedha za kuzijenga kwa kiwango cha lami.
“Vilevile, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara zenye jumla ya kilometa 4,734.43 na madaraja kumi (10) unaendelea. Aidha, miradi ya barabara yenye urefu wa takriban kilometa 5,326.90 na miradi saba (7) ya madaraja ipo katika hatua ya manunuzi kwa ajili ya kufanyiwa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara hizo kwa kiwango cha lami.
“Katika kipindi tajwa madaraja makubwa 9 yamekamilika kujengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni Shilingi Bilioni 381.301 kama ifuatavyo: Gerezani (Dsm), Daraja jipya la Tanzanite (Dsm), Wami (Pwani), Kitengule (Kagera), Kiyegeya (Morogoro), Ruaha (Morogoro), Ruhuhu (Ruvuma), Mpwapwa (Dodoma) na daraja la Msingi (Singida). “Ameeleza Mhandisi Mlavi.
Katika maelezo yake amesema kuwa Madaraja kumi (10) ambayo ni Kigongo Busisi (Magufuli Bridge – Kilometa 3.0), Lower Mpiji (Meta 140), Mbambe (Meta 81), Simiyu (Meta 150), Pangani (Meta 525), Sukuma (Meta 70), Kerema Maziwani (meta 80), Kibakwe (meta 30), Mirumba (Meta 60) na Jangwani (Meta 390) ujenzi wake unaendelea kwa gharama ya Shilingi Bilioni 985.802.
Mhandisi Mlavi amesema jumla ya Madaraja makubwa kumi na tisa (19) yako kwenye maandalizi ya kujengwa ambayo ni: Godegode (Dodoma), Ugala (Katavi), Kamshango (Kagera), Bujonde (Mbeya), Bulome (Mbeya), Chakwale (Morogoro), Nguyami (Morogoro), Mkundi (Morogoro), Lower Malagarasi (Kigoma), Mtera (Dodoma), Kyabakoba (Kagera), Mjonga (Morogoro), Doma (Morogoro), Sanga (Songwe), Kalebe (Kagera), Ipyana (Mbeya), Mkondoa (Morogoro), Kilambo (Mtwara) na Chemchem (Singida).
Katika kipindi cha miaka minne (Juni 2021 Des. 2024) hali ya barabara kuu na zile za mikoa imeendelea kuimarika ambapo barabara zilizo katika hali nzuri na wastani zimekuwa karibu asilimia 90 ya jumla ya mtandao wote wa barabara wenye Kilometa 37,225.72.
ZINAZOFANANA
Mo Dewji: Nikumbukwe kwa kubadili maisha si fedha
Waziri Biteko ahimiza mabadiliko Jeshi la Magereza
Wassira ataja Chanzo cha Deni la Sh. 97 Trilioni.