February 5, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Bilionea na kiongozi wa kiroho Aga Khan afariki dunia

 

BILIONEA  na kiongozi wa kiroho Aga Khan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88, limetangaza shirika lake la hisani la Aga Khan Development Network.
Prince Karim Aga Khan alikuwa imamu wa 49 wa Waislamu wa Ismailia, ambaye nasaba yake inarudi moja kwa moja hadi kwa Mtume Muhammad. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Alifariki dunia kwa amani” mjini Lisbon, Ureno, akiwa amezungukwa na familia yake, shirika lake la hisani lilisema katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii.

Mzaliwa wa Sweden, lakini alikuwa na uraia wa Uingereza na aliishi katika kasri lake Ufaransa.
Misaada ya Aga Khan iliendesha mamia ya hospitali, miradi ya elimu na kitamaduni, haswa katika nchi zinazoendelea.

Aliishi maisha ya kifahari, akiwa na kisiwa cha binafsi huko Bahamas, boti kubwa na ndege binafsi.
Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan ulisema ulitoa “rambirambi zake kwa familia ya Mtukufu na kwa jamii ya Ismailia duniani kote”.

Madhehebu ya Ismailia yana wafuasi wapatao milioni 15 duniani kote, wakiwemo 500,000 nchini Pakistan. Pia kuna idadi kubwa ya watu nchini India, Afghanistan na Afrika.

About The Author

error: Content is protected !!