KATIKA kuboresha elimu nchini Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani amesema kuwa serikali inaangalia namna ya kuboresha maslahi ya walimu ili kada hiyo iendelee kuheshimika na kuthaminiwa kama mama wa taaluma zote Duniani. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Kauli hiyo imeitoa wakati wa hafla fupi ya Uzindizi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2024 iliyozinduliwa leo tarehe 1 Februari 2025 Jijini Dodoma.
Katika uzinduzi huo Samia amesema kuwa ili kutekeleza sera hiyo na mitaala iliyoboreshwa ni lazima kuboresha maslahi ya walimu kwa lengo la kuifanya kada hiyo kuheshimika na kuendelea kuwa na tija kwa jamii.
Kwa kusisitiza jambo hilo Rais Samia amesema kuwa inahitajika hela ya kutosha kuendesha sera hiyo hivyo kinachotakiwa ni kutafuta fedha na fedha inayotakiwa ni nyingi na haiwezekani kuitafuta kutoka kwa wahisani.
“Sera hii haiwezi kutekelezeka kama hakuna fedha na fedha inayotakiwa ni nyingi hivyo sasa nawaagiza watanzania wote kila unachonunua ni lazima kudai risti na anayeuza atoe risti.
“Pia nawaagiza wanaosimamia kodi kuhakikisha mnakusanya fedha kwa uhaminifu hasa kwa ngazi ya Mikoa na wilaya kwa uamninifu mkubwa zaidi ili kufanikisha jambo hilo”amesema Rais Samia.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia Prof. Adrof Mkenda akitoa taarifa fupi kwa Rais Samia amesema kuwa haikuwa kazi nyepesi kupitia mapitio ya sera na miongozo kwani ilitakiwa kuwa fedha nyingi wakati kuna miradi mingi ya maendeleo inayoendelea.
Prof.Mkenda amesema kuwa kitendo cha Rais kuendelea na mapitio ya sera ya elimu ni suala la ujasiri mkubwa na kizalendo na kueleza kuwa kama angekuwa Rais wa kuwaza uchaguzi asingeweza kupitisha jambo hilo.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Jakaya Kikwete katika salamu zake alipendekeza Sera hiyo kuitwa sera ya 2025 kwa kuwa imezinduliwa na Rais Samia.
ZINAZOFANANA
Madeleka ataka maridhiano yatumike kesi ya Dk. Slaa
‘Honey Moon’ yenu ikija na mambo ya hovyo hatukubali – Wassira
Rais Samia kuzindua sera ya Elimu kesho