BARAZA Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limemthibitisha, John Mnyika kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Jina hilo limependekezwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu leo tarehe 22 Januari 2025 ambapo wajumbe wa baraza kuu hilo wakaridhia.
Lissu amesema Mnyika ni mmoja wa wafanyakazi waadilifu ndani ya chama hicho.
Wajumbe watatu pekee ndio walionyoosha mkono wa kutoridhishwa na uteuzi huo lakini Mwenyekiti Lissu akasema wengi wameshinda.
Amani Kolubwa ambaye Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara .
Naye Wakili Ali Ibrahim Juma ameteuliwa na kuthibitishwa na Baraza kuu hilo kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
ZINAZOFANANA
Lissu amteua Dk. Nshala kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Lema na wengine watatu Kamati Kuu
Mbowe aagiza kuunda kamati ya kuponya makovu ya Kampeni
Lissu amzidi Mbowe kura 31, Heche Makamu Mwenyekiti Bara