TUNDU Lissu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewateua wanachama wa chama hicho watano akiwemo Godbless Lema na Dk. Rugemeleza Nshala kuwa wajumbe wa Kamati wa chama hicho. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu alipendekeza majina hayo leo tarehe 22 Januari 2025 mbele ya wajumbe wa baraza Kuu la chama hicho ambao waliwathibitisha kuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho.
Wajumbe walimthibitisha Dk. Nshala kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema na kwamba anakuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.
Baraza hilo limemthibitishaa Lema, Salima Kasanzu, Rose Mayemba na Hafidhi Ali Salehe kuwa Wajumbe wa Kamati Kuu.
ZINAZOFANANA
Mnyika ateuliwa tena kuwa Katibu Mkuu
Mbowe aagiza kuunda kamati ya kuponya makovu ya Kampeni
Lissu amzidi Mbowe kura 31, Heche Makamu Mwenyekiti Bara