BAADHI ya Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya mbalimbali za mkoa wa Kigoma wamesema kuwa msimamo wa kumuunga mkono Tundu Lissu sio wao ni wa Mwenyekiti wa Mkoa huo, Rajabu Bujolwa pekee yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo wameyasema leo tarehe 20 Januari, 2025 jijini Dar es Salaam na baadhi viongozi wa chama hicho kutoka wilaya za Kigoma wamesema wao wanamuunga mkono, Freeman Mbowe na sio Lissu kwenye uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa chama hicho.
Mwenyekiti wa Wilaya Kigoma, Moshi Tabwinke ameseme kuwa yeye na wanachama wa jimbo la Kigoma hawamuungi mkoni Lissu kwa sababu alishindwa kuwanadi wagombea udiwani wa chama hicho Kigoma Mjini.
Naye Heri Chayonga, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Buyungu amesema kuwa hakubaliani na msimamo wa Bujolwa kwa kuwa ni msimamo binafsi na hajawahi kukutana na viongozi wa wilaya wa chama hicho kukubaliana kumuunga mkono Lissu.
ZINAZOFANANA
Mwabukusi: Chadema tutawaadhibu, msipowasiliza wananchi
Rais Samia kwenda na Dk. Nchimbi 2025
Kinana atoa neno baada ya kupatika mrithi wake