
WAKILI Deogratius Mahinyila ameshinda uenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Baraza) kwa kutwaa kura 204 sawa na asilimia 64 huku mpinzani wake Hamis Masoud akiondoka na kura 112 sawa na asilimia 35.3. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Matokeo hayo yametangazwa leo tarehe 14 Januari 2024 na Mwenyekiti wa Uchaguzi huo Elisha Chonya, huku mgombea Shija Shibebeshi alitangaza kujiondoa kabla ya zoezi la kupiga kura halijaanza.
Masoud aliwahi kujipambanua kuwa yeye ni mmoja wa wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Mbowe huku Mahinyila akiwa timu Lissu.
Mkutano wa Bavicha ulianza jana tarehe 13 Januari 2025 .
Mahinyila kwenye kampeni zake alisema kuwa atalifanya baraza hilo kuwa chombo huru cha kuwatetea vijana.
Hata hivyo amesema kuwa ataunda kitengo maalum cha kuhakikisha kuwa hakuna kijana atakayekamatwa na kupelekwa mahakamani kwa sababu za kisiasa
ZINAZOFANANA
Samia: Uhitaji wa kahawa duniani ni fursa kwa Afrika
Shigongo: Tutumie rasilimali zetu kuzibadilisha kuwa fedha
ACT Wazalendo wajifungia kujadili Uchaguzi Mkuu 2025