January 21, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Ushindi wa Profesa Lipumba wapingwa

 

WILFRED Lwakatare aliyekuwa mgombea uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) amesema kuwa hajaridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa CUF yaliyompa ushindi Profesa Ibrahim Lipumba 216.
Lwakatare akihojiwa na Azam TV amesema kuwa amesikitishwa na uendashaji wa uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Vyama vyetu vina matatizo mengi kusema kweli tunainyooshea kidole CCM ikiwa sisi wenyewe tunamatatizo”

Naye mchambuzi wa siasa nchini Dk. Faraja Christomus amesema ushindi wa Profesa Lipumba una shaka kwa kuwa haujafika asilimia 50.

Amesema kuwa Profesa Lipumba amepata Kura 216 sawa na asilimia 36 ya kura zote 592 jambo ambalo lina shaka kwenye mawanda ya demokrasia.

Ameshinda kwa asilimia 36 ushindi uliomzuri uliobeba uwakilishi wa wanachama wengi uwe juu ya asilimia 50 hii inayoonesha hajapata ridhaa ya asilimia 60 ya wapiga kura .

Dk. Christomus amesema kuwa chama hicho kingeupa uzito uchaguzi wa Mwenyekiti na kuipa nafasi demokrasia kingeurudia uchaguzi huo na kwa kuwa shindanisha wagombea walikaribiana kura kwa nafasi chache za juu.

Ameona dosari ya viongozi waasisi wa vyama vya upinzani kushindwa kuwaanda warithi wa nafasi za juu za uongozi

About The Author

error: Content is protected !!