KUTOKANA na uwepo wa magonjwa ya mifugo nchini Tanzania kumesababisha kushindwa kuuza tani 882,182.8 za nyama zenye jumla ya thamani ya USD 3,705,167.76 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 9.3 katika nchi za China, Afrika Kusini, Libya, Umoja wa Falme za Kiarabu, Mauritius na Singapore. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hali hiyo imesababisha sekta hiyo ya mifugo nchi ya Tanzania kutokuwa na mchango mkubwa wa pato la taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mifugo, Dk Ashantu Kijazi alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya mifugo nchini juu wakati wa kongamano la kampeini ya kitaifa ya uchanjaji wa mifugo iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.
Waziri amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe milioni 36.6, mbuzi milioni 26.6, kondoo milioni 9.1, kuku milioni 97.9 na nguruwe milioni 3.7.
Amesema kuwa pamoja na idadi hiyo ya mifugo bado mchango wa sekta ya mifugo kwenye pato la taifa mapaka sasa ni asilimia 6.2. tu.
“Mchango huu ni mdogo ukilinganisha na idadi ya mifugo iliyopo,Moja ya sababu ya mchango wa sekta ya mifugo kuwa mdogo kwenye uchumi wa taifa ni pamoja uwepo wa magonjwa mbalimbali ya wanyama ambayo huathiri uzalishaji wa mifugo kwa kusababisha vifo.
“Lakini pia kusababisha mazao yanayozalishwa kuzuliwa kuuzwa katika masoko ya kimataifa,” ameeleza.
“Kutokana na uwepo wa magonjwa, Tanzania imeshindwa kuuza tani 882,182.8 za nyama; zenye jumla ya thamani ya USD 3,705,167.76 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 9.3 katika nchi za China, Afrika Kusini, Libya, Umoja wa Falme za Kiarabu, Mauritius na Singapore.
“Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kukabiliana na magonjwa ya mifugo juhudi hizo ni pamoja na kuhamasisha uogeshaji wa mifugo kwa kutumia dawa za kuua wadudu kama kupe pamoja na utoaji wa chanjo kwa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo,” ameeleza.
Amesema kuwa kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 mpaka 2023/2024 Serikali imejenga na kukarabati majosho ya kuogeshea mifugo yapatayo 548 na kukarabati majosho 1014 kwa jumla ya shilingi bilioni 11,644.
Alisema kuwa, kiasi cha lita 147.907.75 za dawa ya kuogesha mifugo zenye thamani ya shilingi bilioni 6.7 zilisambazwa kwa gharama ya Serikali.
Alisema juhudi hizi za ujenzi wa majosho, kusambaza dawa za kuogesha mifugo na kuhamasisha uogeshaji zimefanya kupungua kwa vifo vinavyosababishwa na magonjwa yasambazwayo na kupe na wadudu wengiene kupungua kutoka asilimia 72 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 45 mwaka 2024.
ZINAZOFANANA
Waziri Jafo akagua maandalizi miaka 60 ya CBE
TRA, Wafanyabiashara Kariakoo kufanya Bonanza la pamoja J’pili
TMA yatoa taarifa ya uwepo wa Kimbunga Dikeledi, pwani ya Msumbiji