WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa amemuhakikishia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi kuwa Kamati yake ya Uongozi ya maandalizi ya dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 itaendelea kufanya kazi na kutimiza majukumu yake kwa weledi, uaminifu na uadilifu ili kuleta ufanisi kwenye kuijenga Tanzania ambayo watanzania wanaitaka kufikia mwaka 2050. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati wa hotuba yake Visiwani Zanzibar leo Jumatano tarehe 11 Disemba 2024, wakati wa uzinduzi wa rasimu ya kwanza ya Dira 2050, Rasimu iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi.
Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza kuwa kamati yake imetimiza majukumu yake kikamilifu katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kutoa maoni yao kwa njia mbalimbali suala ambalo limefanikisha kuwekwa rekodi ya watanzania takribani 1,170,970 kuweza kufikiwa na kutoa maoni yao kikamilifu.
Majaliwa ametumia sehemu ya hotuna yake pia kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Rais Mwinyi wa Zanzibar kwa maelekezo na miongozo yao ya mara kwa mara suala ambalo limefanikisha Kamati yake ya Uongozi kuweza kutimiza majukumu yake kikamilifu na kwa muda uliopangwa.
ZINAZOFANANA
Mwabukusi: Chadema tutawaadhibu, msipowasiliza wananchi
Mbowe, Lissu wawagawa viongozi wa Kigoma
Rais Samia kwenda na Dk. Nchimbi 2025